Ufafanuzi huo umetolewa leo na mrajisi wa tume ya maendeleo ya ushirika, Tito Haule alipozungumza na blogi hii baada ya kuombwa aeleze sababu za kuzuia mikutano hiyo ambayo ilipangwa kufanyika mwezi huu na hatima ya wajumbe wa kamati za muda za vyama hivyo ambao sio wajumbe wa bodi za vyama vyao vya msingi vya ushirika.
Haule alisema amesimamisha mikutano hiyo kwasababu vyama hivyo bado havijspata usajili wa kudumu kutokana na kutokamilisha baadhi ya vigezo.
Ikiwamo wanachama wake (vyama vya msingi vya ushirika) kuendelea kuwa na hisa kwenye chama kikuu cha ushirika cha cha Ilulu ambacho hadi sasa hakijafilisiwa. "Sasa hapo utaona kuwa wanachama hao wanakuwa wanachama wa vyama vikuu viwili. Jambo ambalo halikubaliki kisheria,kwani majukumu, kazi na wajibu wake unafanana.
Tumewapa miaka miwili wakamilishe taratibu zote ndipo wafanye mikutano hiyo ya mwanzo na chaguzi. Tunazingatia sheria, taratibu na kanuni," alisema Haute . Alisema licha ya Wanachama hao kuwa na hisa kwenye chama cha Ilulu ambacho kipo kwenye mchakato wa kufilisiwa, lakini yapo mambo mbalimbali ambayo vyama hivyo inabidi iyafanye kwa mujibu wa sheria ili vipate usajili wakudumu. Kuhusu wajumbe wa kamati za muda ambao sio wajumbe wa bodi wa vyama vya msingi. Mrajisi huyo alisema kutokuwa wajumbe wa bodi wa vyama vyao vya msingi hakuwaondolei sifa ya kuwa wajumbe wa kamati za muda za vyama vikuu hivyo.
"Kama mjumbe wa kamati aliondolewa kwenye bodi kutokana na ubadhirifu na tuhuma nyingine, huyo hafai kuwa mjumbe wa kamati hizo. Lakini kwakukosa kuwa mjumbe wa bodi tu, wakati bado ni mwanachama wa chama cha msingi anasitshili kuwa mjumbe wa kamati za vyama hivyo, "aliongeza kusema Haule.
Mtaalamu huyo wa ushirika alibainisha kwamba wamevipa usajili wa muda vyama hivyo baada ya kubaini kwamba chama kikuu cha ushirika cha Ilulu haziwezi kuendelea kufanya kazi kwani waliokuwa wanachama wake nihao walioanzisha vya vikuu vya Lindi Mwambao na RUNALI. Hata hivyo wakulima inabidi wahudumiwe.
Alitoa wito kwa vyama vikuu hivyo kukamilisha na kutekeleza maagizo yaliyoagizwa kwa mujibu wa sheria ya ushirika. Ikiwamo sheria namba 6 ya mwaka 2013. Ili viweze kupata usajili wa kudumu na viendelee na taratibu nyingine. Ikiwa nipamoja na chaguzi.
Kufuatia zuio hilo la kutofanyika mikutano ya awali ambayo ingekwenda sanjari na chaguzi. Kuliibuka manung'uniko kutoka kwa baadhi ya wanachana wa vyama vya msingi vya ushirika.
Ambao dhahiri walionesha kutoridhishwa na uamuzi huo wa serikali. Maswali makuu yaliyokuwa ya naulizwa kutoka kwa baadhi ya Wanachama wa vyama vya msingi ni nafasi ya wajumbe wa kamati za muda za vyama vikuu hivyo ambao sio wajumbe wa bodi kwenye vyama vyao vya msingi.
Huku ikifahamika wazi kuwa ujumbe wao kwenye kamati hizo ulitokana na wao kuwa wajumbe wa bodi wa vyama vyao vya msingi. Jambo jingine kwanini vyama hivyo vimepata usajili wa muda vikiwa havina wanachama, na huku vikiwa vimeanzishwa na wanachama.
Vyama vikuu vya ushirika vya Lindi Mwambao na RUNALI vilianzishwa na vilivyokuwa vyama wanachama wa chama kikuu cha ushirika cha Ilulu. Ambapo RUNALI kinaundwa na vyama vya msingi vya wilaya za Nachingwea, Liwale na Ruangwa. Ambapo Lindi Mwambao kinaundwa na vyama vilivyopo katika wilaya za Kilwa na Lindi.
0 comments:
Post a Comment