Thursday, 20 July 2017

Rais Trump ajutia kumteua mwanasheria mkuu Jeff Sessions


Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa hangemteua Jeff Sessions kama mwanasheria mkuu, kama angejua kuwa angejiondoa kutoka kuongoza uchunguzi kuhusu Urusi.

Bwana Trump ameiambia New York Times kuwa hatua ya Bwana Sessions haijakuwa nzuri kwa urais.

Bwana Sessions alijiondoa baada ya kukiri kuwa alikutana na balozi wa Urusi.

Alisema leo Alhamisi kuwa hawezi kujiuzulu na ataendelea kuongoza idara ya sheria vyema.
Bwana Sessions alikuwa mmoja wa wale walimuunga mkono zaidi Bwana Trump.

Licha ya gavana huyo wa zamani wa Alabama kuwa na jukumu la kutekeleza ajenda ya Rais kama mwanasheria mkuu, Bwana Trump mwenyewe anamlaumu wa kuruhusu kuwepo kwa uchunguzi huru ambao umehujumu Urais.

Aliyekuwa mkurugenzi wa FBI James Comey ambaye mwenyewe alilengwa na Trump alifichua kuwa kundi la kampeni ya Trump lilikuwa chini ya uchunguzi.

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment