Monday, 24 July 2017

Polisi yasisitiza kuendeleza mapambano katika uhalifu mwambao wa ziwa victoria


Jeshi la Polisi nchini limesema halitosita kuendeleza mapambano dhidi ya vitendo vya uhalifu vinavyoendelea katika mwambao wa ziwa victoria ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wanaojihusisha na vitendo vya uvuvi haramu katika mwambao wa ziwa hilo.

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP – Simon Sirro amesema hayo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ziara yake mjini Musoma mkoani Mara.

Kamanda Sirro amesema licha kupungua kwa matukio ya uhalifu katika ziwa victoria lakini bado jeshi lake linaendeleza mapambano huku akiwataka wananchi kushirikiana na vyombo vya dola katika kutokomeza kabisa matukio hayo.

Aidha Kamanda Sirro akaagiza kuchukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kupelekwa rumande wale wote watu watakaokutwa na kosa la kutovaa kofia ngumu na hata wanaopakia mshikaki.

0 comments:

Post a Comment