Jeshi la Polisi Temeke jijini Dar es Salaam limeanzisha msako wa wahalifu nyumba kwa nyumba katika Mitaa Mbalimbali ya Temeke
Jeshi hilo likishirikiana na Kamati za Ulinzi za Serikali za Mitaa limeanza kutekeleza Operesheni hiyo ili kumaliza uhalifu.
MAONI YA MWANDISHI.
Nichukue nafasi hii kwanza kulipongeza jeshi la Polisi katika mkoa wa Kipolisi wa Temeke chini ya Kamanda Gilles Muroto Kwa jitihada hizo wanazofanya.
Nibudi Kwa Makamanda wote nchi nzima kuiga mfano huo wa Kamanda Gilles Muroto katika kutekeleza operesheni kama hiyo katika maeneo yao.
Nichukue nafasi hii pia kama mwandishi na mwananchi wa kawaida kuwasihi wananchi wa Temeke na Tanzania Kwa ujumla kutoa ushirikiano Kwa jeshi la Polisi katika kufichua wale wahalifu wote katika mitaa yao.
Alicho kianzisha Kamanda Muroto kinapaswa kupewa ushirikiano wa hali ya Juu kwani wahalifu ni ndugu na jamaa zetu na tunaishi nao katika mitaa yetu na katika majumba yetu pia,huenda akawa baba,kaka,mjomba,binamu,Dada,mama au ndugu Kwa namna yeyote ile.
Nimalize Kwa kusema "Tii Sheria bila Shuruti"
Zaidi Juu ya taarifa mbalimbali tembelea blogu hii ya www.semiosonyo5.blogspot.com na sikiliza kipindi cha Goodmorning Tanzania kila siku Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 06:30asubuhi hadi saa 10:00asubuhi.
Pia kupitia www.radio5fm.co.tz.
Na:Semio Sonyo (blogga)
0 comments:
Post a Comment