Sunday, 2 July 2017

Mkuu Wa Wilaya Ya Kilwa awapiga Kitanzi Walanguzi.

KATIKA kuhakikisha halmashauri ya wilaya ya Kilwa inapata na kuongeza mapato yake ya ndani na serikali kuu inapata kodi kupitia zao la ufuta. Mkuu wa wilaya hiyo, Christopher Ngubiagai ameanzisha operesheni maalumu kwa lengo kukagua vituo na ofisi zinazokusanya ushuru wa zao la ufuta vilivyopo wenye vijiji na halmashauri ya wilaya hiyo, ili kuwabaini wafanyabishara wanaonunua zao hilo bila kulipia kodi na ushuru na wanaotumia mizani zilizokatazwa na wakala wa vipimo  kutokana na kuwaibia wakulima kupitia mizani hizo. 

Akizungumza kwa nyakati na maeneo tofauti, mkuu huyo wa wilaya ambae aliongozana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na wataalamu wa Halmashauri alifanikiwa kuwakamata na kuwalipisha ushuru kwa mtindo wa papo kwa hapo walanguzi, alisema nijambo lisilokubalika kuona serikali kuu, halmashauri na wakulima wanapoteza mapato wakati serikali ipo.

Ngubiagai ambae wilaya yake nimiongoni mwa wilaya zinazo zalisha kwa wingi, zao la ufuta aliongeza kusema hakuna nchi yeyote duniani iliyoweza kuwahudumia wananchi wake na kuwapelekea maendeleo bila kusimamia na kukusanya kodi kwa ufanisi. 

"Wakulima wanadhulumiwa, serikali inakosa  mapato, bei elekezi iliyotangazwa na mkuu wetu wa mkoa, ni shilingi 2000 kwa kila kilo moja. Lakini mnanunua kwa bei ndogo, mnategemea nibaki ofisini, haiwezekani.

Nitawakamata namtalipa kila kinachositahili Kulipwa, "alisema Ngubiagai. Katika ziara ya jana, mkuu huyo wa wilaya alitembelea vijiji vya Nangurukuru, Njinjo, Nasaya, Kandarawe na Chumo.

0 comments:

Post a Comment