Wednesday, 19 July 2017

HISPANIA KAMA BONGO, RAIS WA SOKA ANASHIKILIWA.


Tunatambua kwamba Rais wa shirikisho la soka Tanzania TFF, Jamal Malinzi anashikiliwa kwa tuhuma mbalimbali zikihusu mambo ya fedha. Hali inayofanana na hiyo imetokea huko Ulaya katika nchi ya Hispania.

Taasisi ya kuzuia rushwa ya nchi hiyo iitwayo Unidad Central Operativa imemkamata na kumshikilia Rais wa shirikisho la soka nchini humo Angel Maria Villar na mwanaye anayefahamika kwa jina la Gorka.


Wawili hao wameshikiliwa wakikabiliana na tuhuma mbalimbali za rushwa na matumizi mabaya ya ofisi na taarifa zinasema watafikishwa mahakamani muda wowote.

0 comments:

Post a Comment