Saturday, 1 July 2017

Haijawahi kutokea watu wanagombania kulipa kodi TRA – Rais Magufuli


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa watu kugombania kulipa kodi haijawahi kutokea katika nchi Tanzania, huku akisema kwasasa kila mmoja anataka kwenda kulipa kodi.


Akizungumza leo wakati akizindua rasmi maonyesho ya kimataifa ya Biashara ya Sabasaba, Rais amesema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) tatizo linaweza likawa kwa watendaji wa TRA walivyojipanga kupokea hizo kodi.

“Kwasasa hivi Watanzania wameamka katika suala la kulipa kodi mmeona tu juzi tulivyofanya mabadiliko tu kidogo tu katika kodi za majengo, siku za nyuma TRA walikuwa wanatoa kodi hizo kubwa tu na hakuna mtu aliekuwa anatamani kulipa, sasa wameweka kodi ambayo ni reasonable leo watu wanagombania kulipa kodi haijawahi kutokea katika nchi hii kila mmoja anataka kwenda kulipa kodi ,” amesema Rais Magufuli.

0 comments:

Post a Comment