Akizungumza katika futari iliyoandaliwa na Chuo cha Imam Swadiq, Charles alisema kumekuwa na changamoto nyingi ya kisheria wanapopeleka kesi za mirathi kwa ajili ya kudai haki zao. Alisema kuwa changamoto mojawapo ni rushwa ambapo inawakosesha haki yao ya kugawiwa mali badala yake wanapewa watu wasiostahili pamoja na ucheleweshwaji wa mashauri hayo.
Alisisitiza kuwa wanaamini kupitia serikali hiyo ya Awamu ya Tano hususani Wizara ya Katiba na Sheria itazitatua changamoto hizo kwa wakati ili kuwafanya wajane hao kurudisha matumaini yao yaliyopotea kuhusu haki.
Aidha, amewataka wajane nchini wasijisikie wakiwa, kwani kuwa mjane haina maana kwamba ndio mwisho wa maisha, badala yake waendelee kujituma katika kazi mbalimbali na kupigania haki zao bila kuchoka. Kwa upande wake, Mtumishi wa Chuo hicho, Zaynab Ndete alisema lengo la hafla hiyo ni kuwakutanisha wajane kutoka wilaya mbalimbali za mkoa huo.
Ndete alisema, “Ujane ni suala zito na gumu, katika jamii yetu ya Kitanzania wanawake wengi wanapokuwa wamefiwa na waume zao, wanakuwa katika matatizo makubwa miongoni mwao ni kutengwa au kunyanyapaliwa na familia ya mume kwa kunyang’anywa haki zao za msingi, kunyang’anywa mali zao ambazo wameachiwa kama urithi na waume zao.” Hata hivyo, Ndete aliwaomba wanawake hao kusimama kidete kusimamia malezi ya familia zao kwani jukumu la kuwalea watoto walioachiwa lipo mikononi mwao.
0 comments:
Post a Comment