Tuesday, 20 June 2017

Wahamiaji 120 Wahofiwa Kufariki Baada

Takriban wahamiaji 126 wameripotiwa kupotea baada ya mashua walimokuwa ndani kuzama katika pwani ya bahari nchini Libya .

Taarifa hiyo imearifiwa na shirika la masuala ya uhamiaji (IOM) mapema siku ya Jumanne .

Wakati huo huo msemaji wa IOM alifahamisha kwamba wahamiaji wanne waliweza kuokolewa .

Wengi wa wahamiaji hao ni raia wa Nigeria na Sudan .

Shirika la uhamiaji la UN lafahamisha kwamba takriban wahamiaji 44,209  wameingia Ulaya mwaka 2017 ,wengi wao wameenda Italia ,Ugiriki,Uhispania na Cyprus .

Wahamiaji wasiopungua 966  wamezama na kupotea katika bahari ya Mediterania katika njia inayounganisha Afrika kaskazini na Italia .

0 comments:

Post a Comment