Saturday, 24 June 2017

UCHAGUZI TFF : JINA LA MGOMBEA MMOJA LAKATWA




Wakati majina 73 yakipita katika hatua ya awali, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imechuja jina la Abdallah Mussa katika orodha ya wagombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi ujao wa shirikisho.

Sababu za kukata jina la Mussa ambaye alikuwa anawania nafasi ya Ujumbe kutoka Kanda Na. 1 ya mikoa ya Kagera na Geita ni kutoambatanisha kivuli cha cheti cha kidato cha nne kwa mujibu wa kanuni ya 9 inayozungumzia sifa nane za kuwania uongozi TFF. Katika majina hayo 73, majina 10 ni wale wanaowania urais, makamu rais sita na wajumbe wa kamati ya utendaji 57.

Wagombea wote wanatakiwa kufika kwenye usaili utakaofanyika kuanzia Juni 29, 2017 hadi Julai 1, mwaka huu katika ofisi za TFF Karume, Dar es Salaam kuanzia saa 4.00 asubuhi wakiwa na nyaraka halisi za viambatisho vyote walivyoweka kwenye fomu za maombi. Vyeti vya elimu ya Sekondari viwe vya Baraza la Mitihani (NECTA).

Related Posts:

  • USAJILI:LECEISTER CITY YAMNASA MWENYE EUROPA LIGI TATULeceister,England.MABINGWA wa zamani wa ligi kuu ya soka nchini England,Leceister City wamekiongezea uimara kikosi chao tayari kwa msimu ujao kwa kumsajili nahodha wa Sevilla ya Hispania,Vicente Iborra kwa ada ya £12m.Iborra … Read More
  • TASWIRA NNE ZA DOGO BRADLEY WAKATI WA UHAI WAKEHabari si njema katika familia ya soka ya England na duniani kote, nayo ni kifo cha mtoto Bradley Lowery.Bradley shabiki namba moja wa Sunderland na rafiki namba moja wa mshambulizi mkongwe wa Sunderland na England, Jermain D… Read More
  • KELECHI IHEANACHO AKARIBIA KUTUA LEICESTER CITYKLABU ya Leicester City ipo karibuni kabisa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria, Kelechi Iheanacho kutoka Manchester City, zote za England kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 25, lakini dili hilo linaweza kuchukua… Read More
  • HISTORIA UJERUMANI YATWAA UBINGWA WA MABARA Timu ya taifa ya Ujerumani imetwaa taji la kombe la mabara baada ya kuishinda Chile kwa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Saint Petersburg nchini Urusi. Mshambuliaji Lars Stindl ndie aliyeifungia Ujerum… Read More
  • Tetesi za Soka Ulaya Leo July 02Arsenal wanajiandaa kutoa pauni milioni 125 ili kumsajili Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco na kuwazidi kete Real Madrid (Sunday Mirror).Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amemuambia Alexis Sanchez, 28, kuwa hatojiunga na Manches… Read More

0 comments:

Post a Comment