Uamuzi huo umefikiwa baada ya vikao vyake mfululizo vya Juni 10 na 11, mwaka huu, ambavyo pamoja na uchaguzi wa Lipuli vilijadili na mambo mengine pia.
Uchaguzi huo sasa utafanyika Agosti 5, mwaka huu utasimamiwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kama ilivyopangwa awali na uamuzi huo umezingatia malalamiko yaliyoletwa na wanachama ambao baadhi ya majina yaliyondolewa kwenye daftari la usajili la wanachama.
Tayari Kamati ya Uchaguzi ya TFF iko Iringa kwa ajili ya kutangaza rasmi uchaguzi huo ambako zoezi la kuchukua na kurejesha fomu litaanza Juni 28, mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment