Home »
Kimataifa
» Qatar yaamua kununua ndege za kivita kutoka Marekani

Qatar imetia saini mkataba wa thamani ya dola bilioni 12 kununua ndege za kivita aina ya F-15 kutoka Marekani.
Biashara hiyo ilikamilishwa katika mkutano mjini Washington kati ya waziri wa ulinzi nchini Marekani Jim Mattis na mwenzake wa Qatari.
Hatua hiyo inajiri siku kadhaa baada ya rais Donald Trump kuishutumu Qatari ,mshirika mkubwa wa Marekani kwa kufadhili ugaidi wa kiwango cha juu ,madai ambayo Qatar imekana.
Mataifa mengine ya Ghuba hivi karibuni yalivunja uhusiano wao na Qatar wakiilaumu nchini hiyo kwa kuliyumbisha eneo hilo kupitia ufadhili wake wa makundi yenye itikadi kali na uhusiano wake na Iran.
Qatar ndio taifa lenye kambi kubwa ya majeshi ya Marekani katika eneo la mashariki ya kati ,Al-Udeid .
Kambi hiyo ina takriban wanajeshi 10,000 na ni muhimu katika operesheni za marekani dhidi ya kundi la Islamic state nchini Syria na Iraq.
Matamshi ya rais Trump yalienda kinyume na idara ya ulinzi nchini humo ambayo ilikuwa imeisifu Qatar kwa kuendelea kuimarisha usalama wa kieneo siku chache awali.
Saudia ambaye pia ni mshirika mkuu wa Marekani imeongoza hatua za kutaka kulitenga taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa gesi kuanzia mapema mwezi huu.
Riyadh ilifunga mpaka na anga yake kwa ndege za Qatar Airways huku Bahrain ,UAE na Misri zikivunja uhusiano wao wa kidiplomasia na taifa hilo.
Related Posts:
WHO: Polio yabainika DRCKampeni ya chanjo dhidi ya polio katika mji wa Lubumbashi mwaka 2010.Shirika la Afya duniani (WHO) limetangaza kutokea kwa milipuko miwili ya ugonjwa wa polio nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, miezi michache baada ya … Read More
Watu tisa wauawa katika mlipuko MogadishuTakriban watu tisa wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya bomu lililokuwa limetegwa kwenye gari kulipuka katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.Polisi wanasema gari lililokuwa na bomu hilo lililipuka wakati likielekea k… Read More
Watu watatu wauawa kwa kupigwa risasi MarekaniPolisi wamesema ulinzi umeimarishwa Kwa sasaPolisi katika mji wa San Francisco wamesema watu watatu wameuawa katika shambulio la kufyatua risasi.Mfyatuaji ambaye alikuwa amevalia mavazi ya kampuni moja pia alifariki.Polisi wa… Read More
Moto London: Tunayoyafahamu nini kufikia sasa kuhusu Grenfell TowerWatu 12 wamethibitishwa kufariki na wengine 18 wamo katika hali mahututi hospitalini baada ya moto kuteketeza jumba la ghorofa 24 la makazi magharibi mwa London.Moto huo ulizuka katika jumba hilo usiku wa kuamkia Jumatano.Jen… Read More
Misri yatoa visiwa vyake kwa Saudi ArabiaBunge la Misri limehalalisha Saudi Arabia kumiliki visiwa viwili vya nchi hiyo ambavyo havikaliwi na watu.Mwaka uliopita palitokea maandamano makubwa baada ya serikali ya nchi hiyo kusema kuwa itatoa visiwa hivyo vya Tiran na… Read More
0 comments:
Post a Comment