Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Nyamisi Bahati (27) anayedaiwa kumuua mtoto wake aitwaye Sakimu Hassani baada ya kumtupa ziwa Victoria na kupelekea mtoto huyo kupoteza maisha, tukio analodaiwa kulifanya majira ya saa 1:00 usiku ya tarehe 13/06/ 2017.
Inadaiwa mtuhumiwa ambaye ni mama wa mtoto huyo alitoka nyumbani kwa mumewe na kwenda kuwasalimia wazazi wake akiwa na mtoto wake, lakini baadaye alitoka nje akiwa na mtoto kama anakwenda kumbembeleza ndipo baada ya muda kupita alirudi akiwa hana mtoto na kupelekea Mama yake mzazi wa binti huyo kumuuliza mtoto amemuweka wapi ndipo mtuhumiwa alionekana na mashaka huku akishindwa kuonyesha mahali mtoto alipo na baadaye akasema amemtupa kwenye Ziwa Victoria.
Kamanda Msangi amesema baada ya mtuhumiwa kusema hivyo, Bibi wa mtoto alipiga yowe akiomba msaada kwa watu ili waweze kuja kumuokoa mtoto na wananchi walipofika waliweza kutoa taarifa kituo cha Polisi na kuweza kufika eneo la tukio ambapo walishirikiana na wananchi na kufanya kazi ya kumtafuta majini na baadaye walifanikiwa kumpata ila alikuwa tayari ameshapoteza maisha.
Kamanda Msangi ameendelea kusema kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha mtuhumiwa wa mauaji hayo anasumbuliwa na matatizo ya akili, japokuwa Polisi wapo katika upelelezi na mahojiano na mtuhumiwa pindi uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
Wednesday, 14 June 2017
Mwanza: Mwanamke amtupa mtoto ziwani
Related Posts:
Jela miaka 120 kwa unyang’anyiWATU wawili wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 120 jela baada ya kuopatikana na hatia ya makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha.Waliohukumiwa adhabu hiyo na Mahakama ya Wilaya ya Musoma mkoani Mara ni Nyatali Mashine a… Read More
Mwenyekiti UVCCM Arusha Kufikishwa Mahakamani Kwa Kujifanya Usalaa wa TaifaAliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, UVCCM Mkoa wa Arusha, Lengai Sabaya ambaye ni Diwani wa Sambasha anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kughushi na kutumia kitambulisho cha Usalama wa Taifa.Kamand… Read More
Taarifa Rasmi ya Jeshi la Polisi Kuhusu Wahalifu 13 Waliouawa KibitiTarehe 09.08.2017 majira ya saa 21:00 Hrs (saa tatu usiku) katika mapori ya kijiji cha Rungungu mtuhumiwa akiambatana na Askari Polisi alikwenda kuonyesha Ngome ya watuhumiwa wenzake aliokuwa anashirikiana nao kufanya u… Read More
Dar Yabainika Kuwa Kinara wa Matusi, Mwanza Wizi Imebainika kwamba pamoja na uwepo wa sheria ya makosa ya mtandao lugha ya matusi imeendelea kutumika huku mkoa wa Dar es Salaam ukiwa kinara.Pia Mkoa wa Mwanza nao umebainika kuwa kinara kwa upande wa makosa ya wi… Read More
Magufuli ampiga biti Mbunge CUFRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amempiga biti Mbunge na viongozi wa upinzani mkoani Tanga kutojisifia kuwa wao wameleta m… Read More
0 comments:
Post a Comment