Watu saba wameripotiwa kufariki huku wengine 59 wakijeruhiwa katika mlipuko uliofanyika katika shule ya chekechea nchini China, kulingana na chombo cha habari cha serikali.
Chombo cha habari cha Xinhua kimesema kuwa mlipuko huo ulitokea nje ya shule hiyo katika kaunti ya Fengxian mkoa wa mashariki wa Jiangsu.
Haijulikani ni watoto wangapi walioathiriwa na mlipuko huo.
Sababu ya mlipuko huo haijulikani.
Unaaminika kutokea wakati wazazi walipokuwa wakiwachukua watoto wao nyakati za jioni.
Picha ambazo hazijafanyiwa uhakiki zilionyesha watu wazima waliokuwa wakivuja damu huku watoto wakiwa wamelala ardhini.
Kanda ya video ilionyesha watu waliojeruhiwa wakiwabeba watoto waliokuwa wakilia huku mwanamke mmoja aliyevalia nguo zilizochomeka akionekana kupepesuka.
Watu wawilki waliuawa papo hapo huku wengine watano wakifariki kutokana na majeraha kulingana na Xhinua.
Tisa ya waliojeruhiwa wamedaiwa kuwa katika hali mahututi.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa wameanzisha uchunguzi .
Tovuti ya habari ya China Sohu ilimnukuu mmiliki mmoja wa duka akisema mlipuko mkubwa umesikika ambao anadhani huenda ulisababishwa na kulipuka kwa gesi katika mgahawa mmoja wa chakula.
Thursday, 15 June 2017
Mlipuko waua 7 na wengine 59 wajeruhiwa katika shule ya chekechea China
Related Posts:
Mbunge Bashe Amkalia Kooni JPM, Ahadi ni DeniHUSSEIN Bashe, Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini, mkoani Tabora ameitaka Serikali kutoa kauli juu ya Sh. 200 milioni ambazo Disemba 2016, Rais John Magufuli aliahidi kuzitoa kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya maji katika jim… Read More
Wanawake ACT Wazalendo Wampinga Rais MagufuliRais Atengue Kauli Yake Kuhusu Watoto wa Kike Wanaopata Mimba Mashuleni Maana ni Kinyume na Katiba, Sheria, Busara na hata Ilani ya Chama Chake.Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo imeshtushwa na kusikitishwa sana na tamko la kupi… Read More
Kimenuka:Meya, Madiwani wa Chadema ARUSHA WakamatwaNaibu Meya wa Jiji la Arusha, Viola Likindikoki, pamoja na madiwani wengine wawili wa Chadema wamekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa sababu ambazo mpaka sasa hazijafahamika.Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro amesem… Read More
Vigezo vya kupewa kitambulisho cha UraiaWizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imewatangazia wananchi wote wakazi wa Dar es salaam kuwa watapatiwa ofa maalum ya vitambulisho vya uraia siku ya maonyesho ya sababa ya 41 yanayotarajiwa kufanyikia katika viwanja vya Mwalimu … Read More
Kauli ya Spika wa Bunge Job Ndugai Yalipasua Mbunge Vipande ViwiliDodoma. Kauli ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kuhusu mgawanyo wa bajeti katika majimbo yanayoongozwa na wapinzani imezidi ‘kulipasua’ Bunge baada ya pande mbili za kisiasa kushambuliana ndani ya chombo hicho jana.Jumanne wiki h… Read More
0 comments:
Post a Comment