Friday, 23 June 2017

Mbunge Bashe Amkalia Kooni JPM, Ahadi ni Deni



HUSSEIN Bashe, Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini, mkoani Tabora ameitaka Serikali kutoa kauli juu ya Sh. 200 milioni ambazo Disemba 2016, Rais John Magufuli aliahidi kuzitoa kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya maji katika jimbo hilo,

Bashe ameliambia Bunge kuwa Disemba mwaka jana, Rais Magufuli alitoa ahadi ya Sh. 400 milioni kwa ajili ya kutatua tatizo la maji, Nzega Mjini lakini mpaka sasa ametoa Sh. 200 milioni tu na kumtaka Isack Kamwelwe, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji kueleza ni lini fedha zilizobaki zitatolewa.

“Tulipokea milioni 200 tu, Mhe. Naibu Waziri unawaambia nini Wananchi wa mji wa Nzega juu ya utekelezaji wa fedha iliyobaki ambayo tumekuwa tukisubiri tangu Aprili mwaka huu?” alihoji Bashe.

Ambapo naibu waziri Kamwelwe alijibu akisema, “Ni kweli Rais alitoa ahadi ya kupeleka milioni 400 kwa ajili ya kuboresha huduma ya maji katika Mji wa Nzega. Milioni 200 tumeshaikabidhi Mamlaka ya Maji ya Tabora na tutapeleka fedha zilizobaki siku za hivi karibuni.

Kamwelwe alisema kupitia mradi mkubwa wa maji wa kutoka Solwa kwenda Nzega na Tabora  uliosainiwa hivi karibuni miundombinu itakarabatiwa.

Kwa upande wake John Mnyika Mbunge wa Kibamba, swali lake liliulizwa na Mbunge wa Vunjo, James Mbatia ambapo lilihoji;

“Jimbo la Kibamba linapaswa kuhudumiwa kwa sehemu kubwa na maji ya kutoka mtambo wa Ruvu Juu, je ni kwanini miradi ya maji imechelewa kukamilika kinyume na ratiba inayotolewa  na Serikali?” alihoji na kujibiwa;

“Maeneo yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu Juu ni pamoja na Mlandizi, Visiga, Picha ya Ndege, Tumbi na Pangani.
“Maeneo haya yataanza kupata maji baada ya kukamilika kwa mradi wa mfumo wa kusambaza maji ambao unaendelea kutekelezwa na kampuni ya Jain Irrigation System Ltd.”

Related Posts:

  • Makosa dhidi ya binadamu yaongezeka kwa asilimia 0.9Jeshi la Polisi limesema makosa dhidi ya binadamu yanayojumuisha mauaji, kubaka, kulawiti, kunajisi, wizi na kutupa watoto na usafirishaji binadamu yameongezeka nchini.Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert … Read More
  • Njombe yaongoza maambukizi ya UKIMWIWaziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango leo Disemba 2017, amemkabidhi Rais John Pombe Magufuli   takwimu inayoonyesha  hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU), wakati wa uwekaji wa jiwe  la msi… Read More
  • Wanaohubri kwenye mabasi kukiona cha motoBaraza la Ushauri wa watumiaji wa huduma za safiri wa nchi kavu na majini, SumatraCCC limekitaka chama cha wamiliki wa mabasi nchini TABOA na washirika wao kuhakikisha wanasimamia vyema suala la baadhi ya watu kugeuza magari … Read More
  • NHC YATOA KIWANJA KWA JESHI LA POLISI ENEO LA SAFARI CITYNa Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi ArushaShirika la Nyumba la Taifa (NHC) limetoa eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 5000 kwa Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi na nyumba za askari katika en… Read More
  • Kinana awapa somo viongozi waliochaguliwaCHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimewataka viongozi wake wote waliochaguliwa hivi karibuni katika ngazi mbalimbali kuhakikisha wanawatumikia wanachama na wasio wanachama kwa uadilifu na uzalendo ili kuendelea kukijengea imani C… Read More

0 comments:

Post a Comment