Wednesday, 21 June 2017

Kufuatia mzozo wa Ghuba, Saudi Arabia yawafukuza ngamia wa Qatar


Ngamia zinazomilikiwa na Qatar pia zenyewe zimejipata katikati ya mzozo wa ghuba baada ya Saudi Arabia kutoa amri ya kuondolewa kwa mifugo hiyo nchini humo.

Ngamia hizo zilisalia mpakani mwa Qatar na Saudia Arabia bila ya maji wala chakula kwa siku kadhaa kufuatia amri ya kufukuzwa kutoka kwa nchi hiyo.

Qatar ilichukua hatua ya kuunda makaazi ya dharura ya ngamia hizo huku ikitayarisha kufanya usafirishaji wa wqanyama hao.

Siku ya Jumanne maelfu ya ngamia zilipitishwa mpakani na kusafirishwa kuelekea Qatar ambapo zilikutanishwa na wenzao nchini humo.

Ni wiki tatu sasa tangu mzozo wa Qatar kuanza ambapo mataifa ya kiarabu yaliwekea vikwazo nchi hiyo na kukata uhusiano kwa madai kuwa Qatar inaunga mkono makundi ya kigaidi.

Hadi kufikia sasa Qatar inakataa madai hayo .

0 comments:

Post a Comment