Tuesday, 13 June 2017

Jinsi ya kujiukinga na ugonjwa wa kaswende


Ugonjwa wa kaswende ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na bakteria aina ya Treponema pallidum.  Ugonjwa wa huu ni kati ya magonjwa ya zinaa yanayoongoza kwa kusababisha madhara mengi. 
Maambukizi ya kaswende wakati wa ujauzito huleta madhara mengi sana, mfano wa madhara hayo ni kujifungua kiumbe ambacho kimeshakufa, mtoto kuathirika na ugonjwa huu wakati wa kuzaliwa, mtoto kupata matatizo wakati wa   ukuaji wake, degedege na kuongezeka kwa vifo vya watoto wachanga nchini. 
Hivyo watalamu mbalimbali wa masuala ya afya wanasshauri ya kwamba kabla mama mjamzito hajajifungua ni vyema akatibu ugonjwa huu wa kaswende mapema zaidi, kwani endapo utachelewa unaweza ukasababishia kijacho magonjwa ambayo yamekweisha orodhoshwa hapo juu. 
Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa kaswende
Kufanya ngono salama kwa kutumia kondomu, hii ni  njia sahihi ya kuepuka ugonjwa kaswende pamoja na magonjwa yote ya tokanayo na ufanyaji zinaa. 
Kama umepata ugonjwa huu hakikisha haufanyi tena ngono, hasa ngono zembe mpaka pale utakapokuwa umemaliza tiba ya magonjwa za sinaa mathalani ugonjwa wa kaswende. 
Kwa wajawazito ambapo wanamaambukizi ya ugonjwa wa kaswende ni vyema, wakahakikisha  wanahudhuria a kliniki mapema ili kama ukigundulika kuwa na kaswende hivyo kupata tiba haraka. 
Epuka kugusana na majimaji yoyote yanayotoka kwa mtu aliyeathirika kwa ugonjwa huu. 

0 comments:

Post a Comment