Sunday, 18 June 2017

"Vijana jiepusheni na ugaidi"- Kiongozi mkuu shia Tz


"Vijana ni Tunu na nguzo ya Taifa, Taifa lolote duniani haliwezi kustawi pasipo mchango wa vijana kwani wao wanakuwa na fikra pevu na uwezo wa kuchanganua mambo kwa haraka zaidi kuliko wazee."

Hayo yamesemwa jana Jioni na Kiongozi mkuu wa dhehebu la Shi- Ithnaasheria Tanzania kwenye Semina iliyoandaliwa na Masjid Al Qadir uliopo Kigogo Dar es salaam, Semina hiyo ilijumuisha Vijana wanaoishi maeneo ya Kigogo na sehemu nyingine za karibu na Msikiti huo.

 Wawezeshaji wa semina hiyo ni Shariff Sagaff Ahmed kutoka Maande Islamic Centre akishirikiana na Mwalimu Kassim Hassan kutoka Shule ya sekondari ya Kibondo liyopo Kigoma na mwenyeji wao akiwa ni Sheikh Hemed Jalala. Kwenye Semina hiyo vijana walipewa elimu ya kujitambua na kufahamu nini majukumu yao kama vijana na kwa kiasi gani wanaweza kujiepusha na mambo ya anasa na kuwa na bidii kwenye kazi.

Pasipo kuangalia itikadi za kidini walialikwa vijana wa dini zote na walipewa elimu ya kumjua mungu kila mmoja kwa imani yake na kuepuka vishawishi na kazi zote za muovu Shetani. Pia sheikh Hamed Jalala alipenda kuwahusia vijana kutojihusisha na makundi mabaya kwani tatizo la ukosefu wa ajira isiwe kigezo cha wao kujihusisha na shughuli za ugaid pamoja na ujambazi ambao tunaona ukishamili kwa kwa kasi na watendaji wa hayo yote wakiwa ni vijana.

Na mwisho kabisa vijana hao walipata Futari kwa pamoja na Sheikh Mkuu wa dhehebu hilo la Shia Hemed Jalala pamoja viongozi wengine wa msikiti huo

0 comments:

Post a Comment