Thursday, 22 June 2017

Haya Ndio Madhara 6 Ya Kutoa Mimba


Kutoa mimba ni nini? Hii ni hali ya mwanamke kwa hiari yake mwenyewe kuharibu mimba iliyoingia ndani ya kizazi chake.

Kutokana kuongezeka kwa idadi ya mahusiano duniani na kutotumia njia za uzazi wa mpango kwa watu wengi walioko kwenye mahusiano, wasichana wengi kwa sasa wanatoa mimba.
Utafiti nilioufanya mwenyewe nimegundua kwamba zaidi ya asilimia tisini ya wasichana wanaokua kwenye mahusiano na wanaume zaidi ya mwaka mmoja kabla ya ndoa hutoa mimba na asilimia tano tu ya wote ndio wanaamua kuzaa. Sio ajabu kusikia mtu ameolewa akiwa ametoa mimba nne mpaka tano. Sasa unajiuliza bado kuna mtu humo au mfu?

Hata hivyo hao wanaozaa pia hujikuta wamebeba mimba zingine wakati watoto wao wakiwa wadogo na kulazimika kuzitoa. Najua watu wengi wanatoa mimba kukwepa aibu, kutokua tayari kisaikolojia na kadhalika lakini ni bora kutumia njia za uzazi wa mpango kama condomu kuzuia mimba na kama kondomu huiwezi basi tumia njia zingine kama sindano na vijiti kwasababu wengi wenu mkishalewa pombe au kondomu isipokuepo ndio basi tena.

Hebu tuyaangalie madhara ya kutoa mimba kama ifuatavyo…

Uwezekano mkubwa wa kufa:
Utafiti uliofanywa na madaktari wa finland mwaka 1997 umegundua kwamba wanawake wanaotoa mimba wanauwezekano wa kufa mara nne zaidi kuliko ambao hawatoi mimba. Vifo hivyo vimekua vikisababishwa na kujiua wenyewe kutokana na kujuta kwa maamuzi yao na madhara ya mda mrefu ya kimwili yatokanayo na kutoa mimba. Vifo ndani ya wiki moja baada ya kutoa mimba hutokana na kuvuja damu sana, madhara ya dawa za usingizi, mabonge ya damu kwenye mishipa ya damu na mimba iliyotunga nje ya uzazi. Utafiti pia uliongeza kutoa mimba moja uwezekano wa kufa unakua 45%, mimba mbili 114%, mimba tatu 192%.

Ugumba kwa wanawake wengi:
Miaka hii ya karibuni wanawake wengi ambao wanalia kutopata watoto wana historia za kutoa mimba miaka iliyopita, na wengi wao nilionana nao wanajuta sana kwa maamuzi yao. Hii inatokana na madhara makubwa waliyoyapata kwenye mfuko wa uzazi baada ya mimba kutoka.

Mimba kutunga nje ya kizazi:
Mfuko wa uzazi una utando maalumu amaboa hufanya mimba iliyotungwa kwenye mirija iitwayo fallopian kuwezesha yai kushuka hadi kwenye mifuko ya uzazi. Lakini utoaji wa mimba huambatana na magonjwa ya mirija hiyo na kupoteza utando huo na kusababisha mimba kukulia huko.matibabu ya tatizo hili ni kukata mrija husika tu hivyo kuongeza hatari ya ugumba..

Kuzaa watoto wasio na akili nzuri:
Utoaji wa mimba kuharibu mlango wa mfuko uzazi kushindwa kushika vizuri na matokeo yake mwanamke huyu hujikuta akizaa kabla ya mda husika akibeba mimba nyingine. Lakini pia watoto hawa wanaozaliwa kabla ya muda maalumu  na viungo ambavyo havijakomaa hupata shida ya ubongo na kua wagonjwa wa akili maisha yao yote.

kansa ya mlango wa uzazi
Wanawake wanaotoa mimba wana hatari kubwa ya kupata kansa ya mlango wa uzazi kuliko wengine ambao hawajatoa mimba. Hii ni kwasababu ya kusumbuliwa kwa mlango huo kwa dawa za kutoa mimba, vifaa vya kutoa mimba na mabadiliko ya ghafla ya homoni za uzazi.

Kuathirika kisaikolojia;
Hakuna mwanamke ambaye hatakaa ajutie maamuzi yake ya kutoa mimba siku za usoni hata kama hakupata madhara yeyote hii itamfanya aishi kama ana deni Fulani maisha yake yote na itakua inamuumiza usiku na mchana. Zingine ni kukosa hamu ya kula, kusikia sauti ya mtoto anayelia wakati hayupo, kua na hasira sana…

Mwisho
kumbuka kila mwaka wanawake 70000 wanakufa kwa kutoa mimba...maumivu ya kukosa mtoto ni makali sana kuliko aibu ya kuzaa nje ya ndoa. Hawa wanaozaa sasa hivi unawaona malaya ipo siku utawakumbuka utakapo ambiwa na daktari kwamba labda itokee miujiza ndo utazaa.Kama hutaki mimba tumia njia za uzazi wa mpango kwani kuendelea kutoa mimba kutakupa adhabu ya kukosa mtoto ambayo adhabu hiyo utaitumikia maisha yako yote.

Related Posts:

  • Madhara ya kuvuta SigaraUfutaji sigara huathiri mwili kwa njia tofauti na madhara yake ni makubwa kiafya. Inakadiriwa kuwa, hadi sasa kumegunduliwa kemikali zipatazo 7,000 katika moshi wa sigara ambapo 250 kati ya hizo ni sumu na 70 zinasababisha ka… Read More
  • Madhara Ya Kuangalia Video Za Ngono (Porn) Na Namna Ya KuachaKuangalia video za ngono sio jambo jipya kwa jamii yetu, kimsingi ni watu wachache sana wanaweza kujizuia kujichua au kupiga punyeto baada ya kuangalia video za ngono.Bahati mbaya tabia ya kuangalia video hizi watu wengi huip… Read More
  • Namna Ya Kuishi Na HIVTarehe 1 desemba kila mwaka, ni siku ya ukimwi duniani.Ukimwi na magonjwa mengine makubwa yamepewa siku rasmi kila mwaka ili kuikumbusha jamii juu ya mapambano dhidi ya magonjwa hayo. Katika siku hizo pia hutolewa matokeo ya … Read More
  • Tambua Madhara ya Ulaji wa ChipsiChips ni aina ya chakula ambacho hupendwa na watu wengi na pia ni miongoni mwa vyakula vyenye mafuta mengi. chips pia inasemekana ni miongoini mwa vyakula ambavyo hupikwa katika joto la juu zaidi ya 300 degree.Chips ni chakul… Read More
  • Faida nyingine ya kutumia PapaiWakati mwingine tunashauriwa kutumiwa kutumia matunda kwa wingi kwani matunda ni mbadala wa tiba ambazo zinapatikani mahospitallini. Hata hivyo kama ulikuwa hujui ni kwamba matunda yana vitamin ambavyo ni muhimu katika mwili … Read More

0 comments:

Post a Comment