Michuano ya Confedaration Cup iliendelea kupigwa hii leo nchini Urusi ili kutafuta timu mbili za kuungana na Ureno na Mexico kwa ajili ya kucheza nusu fainali ya michuano hiyo.
Katika mechi za leo ilishuhudiwa Cameroon wawakilishi wa Afrika wakiyaaga mashindano hayo baada ya kukubali kipigo cha mabao mawili kwa moja toka kwa miamba ya Ujerumani.
Baada ya kipindi cha kwanza kuisha kwa suluhu ya bila kufungana, kipindi cha pili dakika ya 48 Ujerumani waliandika bao la kwanza kupitia kwa Kerem Dermirbay kabla ya Timo Werner kufunga mara mbili.
Bao la kufutia machozi la Cameroon lilipatikana kunako dakika ya 79 baada ya mchezaji wa Ujerumani Marc Stegen kujifunga akiwa katika hatihati za kuokoa shambulizi.
Chile nao iliwabidi kufanya kazi ya ziada baada ya Martin Rodriguez kuwasawazishia bao dakika ya 61 ikiwa ni goli la kusawazisha baada ya lile la James Troisi alilowafungia Australia dakika ya 42.
Kwa matokeo hayo Ujerumani wamefikisha alama 7 na wanaongoza kundi hilo huku Chile nao wakifudhu baada ya kufikisha alama 5 na kumaliza katika nafasi ya pili.
0 comments:
Post a Comment