Saturday 17 June 2017

Mwanajeshi wa Afghanistan awashambulia wanajeshi wa kigeni


Mwanajeshi wa Afghanistan awashambulia wanajeshi wa kigeni


Mwanajeshi moja wa Afganistan ameshambulia vikosi vya kigeni katika kambi ya kijeshi ambapo wanajeshi kadha wa Marekani wameuawa.

Shambulio hilo lilitokea katika kambi iliyo kaskazini mwa nchi siku ya Jumamosi.


Hata hivyo msemaji wa jeshi la Marekani katika mjini Kabul alitupilia mbali madai ya awali kuwa wanajeshi wa Marekani walikuwa wameuawa.

Walisema kuwa idadi fulani ya wanajeshi walijeruhiwa wakati mwanajeshi huyo wa Afghanistan alifyatuliwa risasi.


Mazar-e Sharif , Afghanistan


Iliripotiwa kuwa mwanajeshi mmoja wa Afganistan aliuawa na mwingine kujeruhiwa wakati wa kisa hicho.

Kambi hiyo iliyo kaskazini mwa mkoa wa Mazar-e Sharif ni makao ya wanajeshi 209


Kisa hicho kinatokea wiki moja baada ya komando mmoja wa Afganistan kuwauwa wanajeshi 3 wa Marekani mashariki mwa Afghanistan.

Taliban walidai kuhusika kwenye shambulizi hilo.

0 comments:

Post a Comment