Saturday 17 June 2017

Malkia Elizabeth: Kuna majonzi kufuatia majanga yaliyoikumba Uingereza


Malkia akikutana na waathiriwa wa moto


Malkia Elizabeth wa Uingereza amesema ni vigumu kuepuka majonzi kufuatia kile alichosema ni msururu wa majanga yaliyokumba taifa hilo hivi karibuni.


Malkia akiwa na wananchi


Katika ujumbe wa kuadhimisha rasmi siku yake ya kuzaliwa, malkia amesema watu wa nchi hiyo wameonyesha mshikamano licha ya changamoto zinazoikabili.


Grenfell Tower


Serikali ya Uingereza imesema itafanya kila iwezalo kurejesha imani ya walioyonusurika mkasa wa mbaya wa motokayika jengo la Grenfel Tower mjini London.


Waandamanajimjini London wakitaka hatua kuchukuliwa


Hii ni baada ya waziri mkuu Bi Theresa May,kuzomewa na waandamanaji waliyokuwa na ghadhabu. Watu thalathini wamethibitishwa kufariki katika mkasa huo.


Huenda manusura wasipatikane


Hotuba ya Malkia Elizabeth inafuatia shabulizi la kigaidi la mwezi uliyopita mjini Manchester na pamoja na lile la London Bridge. 


0 comments:

Post a Comment