Saturday 17 June 2017

Mali yataka UNSC kuidhinisha haraka makubaliano ya nchi za G5 dhidi ya wanajihadi


Rais wa Mali Ibrahim Boubakar Keïtaakiwa narais wa Ufaransa Emmanuel Macron mjini Gao Mei 17 2017.


Waziri wa mambo ya kigeni nchini Mali jana Ijumaa amelishinikiza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha haraka azimio la kuundwa kikosi maalum kwa ajili ya kupambana makundi ya kijihadi ambayo yanazidi kukabili nchi hiyo ya ukanda wa Sahel.

Waziri, Abdoulaye Diop, ameelezea wasiwasi mkubwa wa Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita, ambaye anaongoza muungano wa kikanda wa nchi tano zinazojulikana kama G5 za ukanda wa Sahel,kuhusu ugumu unaochelewesha kuidhinishwa kwa azimio hilo.

Amewataka wajumbe wa umoja huo kupitisha azimio hilo bila kuchelewa.

Kundi la G5 linalojumuisha nchi za Mali , Chad, Mauritania na Burkina Faso, zilikubaliana mwezi Machi kuunda kikosi imara cha askari elfu tano ili kukabiliana na wanajihadi lakini linangoja idhini ya Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa kabla ya kutekeleza azma hiyo.

0 comments:

Post a Comment