Saturday 17 June 2017

Chama tawala Rwanda chamuidhinisha raisi Kagame kuwa mgombea wake wa uchaguzi ujao


           Raisi wa Rwanda Paul Kagame


Chama tawala nchini Rwanda RPF kimemuidhinisha raisi Paul Kagame kuwa mgombea wake wa uraisi katika uchaguzi wa mwezi August mwaka huu.

Hatua hii inakuja baada ya baadhi ya vyama vya upinzani Kutangaza kumuunga mkono raisi Kagame.

Uchaguzi utafanyika mapema mwezi wa nane huku kampeni zikitarajiwa kuanza mwezi ujao Julai.

hatua ya Wabunge nchini Rwanda kupitisha muswada utakaoidhinisha kubadilishwa kwa vipengee vya katiba vitakavyoruhusu rais Paul Kagame kuongoza kwa muhula wa tatu.

Takribani Miaka miwili iliyopita Rwanda katika baraza la seneti na bunge ulipitishwa muswada ulioidhinisha kubadilishwa kwa vipengee vya katiba kuruhusu rais Paul Kagame kuongoza kwa muhula wa tatu kama hatua ya mwanzo kuelekea kufanyika mabadiliko ya katiba.

Mamilioni ya raia nchini Rwanda walitia sahihi pendekezo la kumtaka rais Kagame kuendelea kuongoza taifa hilo hata baada ya kukamilika kwa muhula wake wa pili.

0 comments:

Post a Comment