Wednesday 14 June 2017

Kiranja wa Bunge la Marekani Steve Scalise apigwa risasi


Kiranja wa walio wengi Bungeni Steve Scalise 


Kiranja wa walio wengi katika Bunge la Congress nchini Marekani Steve Scalise, amepigwa risasi na kujeruhiwa alipokuwa akihudhuria mazoezi ya mchezo wa baseball miongoni mwa wabunge.

Yamkini watu wawili wamejeruhiwa, katika kile mashuhuda wanasema kuwa kisa cha umiminunaji wa risasi katika jimbo la Virginia mapema leo Jumatano.

Seneta wa Republican, Rand Paul, anasema kuwa alisikia mlio wa risasi ya kwanza, kisha ikafuatiwa na milio ya risasi.

Walinda usalama walijibu mashambulio hayo. 


Ramani ya jumbo la Virginia.



Bwana Scalise ambaye ni mwanachama wa chama cha Republican, anasemekana alipigwa risasi kwenye makalio, huku ikisemekana kuwa afya yake haimo hatarini kwani amefikishwa hospitalini kwa matibabu pamoja na walinzi wake ambao pia walijeruhiwa na mshambuliaji.

Idara ya Polisi huko Virginia, inasema kuwa imemtia mbaroni mshambuliaji. 


Mbunge Ruben Kihuen‏ aliweka kwenye mtandao wa tweeter picha hii ya wabunge wa Democratic, wakiwaomba manusura wa mshambuliaji huyo 


Rais Donald Trump amesema kuwa: "Tumetamaushwa mno na janga hilo."

Katibu wa mawasiliano wa Ikulu ya White House , Sean Spicerameandika katika mtandao wa kijamii wa tweeter kuwa Rais Donald Trump anajulishwa kuhusiana na shambulio hilo.

0 comments:

Post a Comment