Saturday 17 June 2017

DIWANI WA KIVUKONI AUNGA MKONO JESHI LA POLISI KWA PIKIPIKI


Diwani wa Kata ya Kivukoni, Henry Massaba ametoa pikipiki mbili kwa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kati zenye thamani ya sh. Milioni Tano ili ziweze kutumika kwa masuala ya usalama kwa wananchi wa kata hiyo Kivukoni.

Akizungumza wakati wa kukabidhi pikipiki hizo , Massamba amesema kuwa kumeibuka wizi wa kutumia pikipiki hivyo hata polisi wanatakiwa kutumia pikipiki kwa ajili ya kuwakimbiza wahalifu hao.

Massamba amesema kuwa wahalifu wamekuwa na njia tofauti za kufanya uhalifu na kuamua kutumia pikipipiki kwa kutambua hawawezi kukamatwa kutokana na polisi kwa muda mwingi wanatumia magari.

Aidha amesema kuwa ataendelea kushirikiana na jeshi la polisi kwa namna juu ya kuhamasisha masuala ya ulinzi ili wananachi waishi kwa amani pamoja na mali zao.

Nae Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kati , Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Amon Kakwale amesema kuwa msaada huo ni mkubwa na kuwataka watu wengine waendelee kuliunga mkono jeshi la polisi.

Kakwale amesema kuwa Diwani wa Kata ya Kivukoni amejitoa kwa ajili ya wananchi kuweza kupata usalama.


Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kati , Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Amon Kakwale akizungumza wakati hafla ya kukabidhiwa pikipiki mbili zilizotolewa na Diwani wa Kata ya Kivukoni leo jijini Dar es Salaam.

Diwani wa Kata ya Kivukoni, Henry Massaba akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi pikipiki kwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kati katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Diwani wa Kata ya Kivukoni, Henry Massaba akikabidhi msaada wa Pikipiki Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kati Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Amon Kakwale katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Sehemu Polisi wa Wilaya ya Kati pamoja na wananchi wa kata ya kivukoni wakiwa katika hafla ya kukabidhiana Pikipiki iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

0 comments:

Post a Comment