Thursday 15 June 2017

Wananchiawasusia zahanati, Nachingwea



Anaripoti Ahmad  Mmow kutoka Nachingwea 

URASIMU usionasabu na usumbufu wanaopata wananchi kwenye zahanati za serikali, kumetajwa kusabanisha wananchi kukimbilia kutibiwa kwenye hospitali ya wilaya ya Nachingwea.

 Hayo yameelezwa leo kijijini Mpiruka wilaya Nachingwea na baadhi ya Wanachama wa chama cha msingi cha Ukombozi waliopo kwenye mfuko wa bima ya afya (CHF).

Wakizungumza kwenye mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika katika kijiji cha Mpiruka A, walisema ingawa wanatambua kuwa sheria in inawata 
                     
waanze kwenda zahanati kabla ya kwenda katika hosipitali ya wilaya, lakini usumbufu wanaopata kutoka kwa baadhi ya wahudumu wa zahanati za serikali unawafanya wakimbilie katika hosipitali ya wilaya huku wakiwa hawana barua za rufaa zinazotoka kwenye zahanati.

Mwanahawa Kinunda ambae nimiongoni mwa wanachama 535 waliolipiwa na chama cha msingi Ukombozi kuingia kwenye  mfuko wa bima ya afya, alisema baadhi ya wahudumu wa zahanati wamekuwa wakitengeneza urasimu unaosababisha usumbufu kiasi cha kuwacheleweshea matibabu.

Alisema licha ya usumbufu lakini pia wamekuwa na lugha za kuhudhi kwa wagonjwa na ndugu wa wagonjwa wanaowapeleka kwenye zahanati hizo. "Sisi tunajua kwamba tunatakiwa tuanze kwenda zahanati ndipo twende hospitali ya wilaya, tena tukiwa na barua za kutoka zahanati.

Lakini hatushugulikiwi ipasavyo, urasimu ni mwingi lugha chafu tutaona bora twende hosipitali ya wilaya hatuwezi kuteseka wakati hosipitali ya wilaya ipo, "alisema Mwanahawa. Mwanachama mwingine, Amidu Cbipela licha ya kulaumu urasimu usio na sababu unaofanywa na baadhi ya watumishi wa zahanati na hosipitali kwa wananchi walipokwenye mpango wa bima ya afya. Lakini pia hawapati huduma zinazo sitahili. Kwamadai kuwa dawa nyingi wananunua kutoka kwenye maduka ya dawa.

 "Huku kwenye zahanati hali ndio hiyo, tukienda hosipitali ya wilaya dawa tunaambiwa tukanunue madukani.

 Nae mwanachama Steven Chitalo alitoa wito kwa maofisa wa mfuko wa bima ya afya kuainisha nakuweka wazi ni aina gani za matibabu na magonjwa gani yanasitahili kutibiwa kupitia bima ya afya. Kwamadai kuwa kuna mkanganyiko mkubwa unaosababisha waliopo kwenye mpango huo kushindwa kujua. Chitalo alitolea mfano huduma za upasuaji. Ambapo alisema baadhi ya wanachama wa mfuko huo wanalipa takribani shilingi 150, 000  ili wafanyiwe upasuaji. Akijibu malalamiko ya wananchi na wanachama wa chama hicho cha msingi chenye wanachama 851.


Mratibu msaidizi wa mfuko wa bima ya afya, Bahati Meshack alitoa wito kwa wananchi kutokubali kuwapa fedha wauguzi, waganga na madaktari wanapokwenda kwenda kupata huduma. Badala yake walipie kwa kuzingatia taratibu, kanuni na sheria.

Pia wahakikishe wanapewa stakabadhi halali baada ya kufanya malipo. "kuhusu kuainisha aina za matibabu na magonjwa tumefanya hivyo, hawa viongozi wenu wanayo orodha," alisema Bahati. aidha aliwataka kupeleka malalamiko dhidi ya vitendo viovu vya baadhi ya wahudumu,kwani dhamira ya serikali nikuwapa huduma wananchi bila usumbufu na manyanyaso.

 Huku akiwatoa hofu kuwa serikali inadhamira ya kuwapatia matibabu kamili. Bali nyakati fulani aina ya dawa huwa hazipo, kwasababu huwa zinakosekana hata bohari kuu ya dawa (MSD).Chama cha msingi Ukombozi kimemudu kuwaingiza na kuwalipia wanachama wake 535 kati ya 851 kwenye mpango wa matibabu kupitia bima ya afya. Huku wanachama wanachama waliosalia wanatarajiwa kuingizwa hivi karibuni.

0 comments:

Post a Comment