Thursday 15 June 2017

UJENZI WA MAEGESHO YA KIVUKO CHA LINDI NA KITUNDA WAANZA


Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Lindi Mhandisi Margwe Boay (wa kwanza kulia) akielekeza jambo wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa maegesho ya kivuko kati ya Lindi na Kitunda unaoendelea mkoani hapo, wa pili kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu. Serikali inatarajia kupeleka kivuko eneo hilo mara baada ya ujenzi wa maegesho hayo kukamilika.


Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle (wa nne kulia) akisisitiza jambo wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa maegesho ya kivuko kati ya Lindi na Kitunda unaoendelea mkoani Lindi, kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu.


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu (wa pili kushoto aliyenyoosha mkono)  akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa maegesho ya kivuko kati ya Lindi na Kitunda unaoendelea mkoani Lindi. Serikali inatarajia kupeleka kivuko mara baada ya ujenzi wa maegesho hayo kukamilika.


Mkandarasi wa kampuni inayojenga maegesho ya kivuko kati ya Lindi na Kitunda Mhandisi Emmanuel Lyimo (wa kwanza kulia) akimuelekeza jambo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa maegesho unaoendelea mkoani Lindi. Serikali inatarajia kupeleka kivuko mara baada ya ujenzi wa maegesho hayo kukamilika.


Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Lindi Mhandisi Margwe Boay (wa pili kulia) akielekeza jambo wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa maegesho ya kivuko kati ya Lindi na Kitunda unaoendelea mkoani hapo, wa pili kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu.

PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA).

………………………..

LINDI

Mkandarasi aliyepewa kazi ya ujenzi wa maegesho ya kivuko katika maeneo ya Lindi na Kitunda tayari ameanza kazi hiyo na anatarajia kuikamilisha ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu. Akikagua maendeleo ya ujenzi huo, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu amemtaka Mkandarasi huyo kuhakikisha anamaliza kazi hiyo mapema iwezekanavyo hata kabla ya muda uliopangwa ili wananchi wa maeneo ya Lindi na Kitunda waanze kupata huduma ya kivuko. Amesisitiza kuwa Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuondoa kero ya usafiri kwa wakazi wa maeneo hayo hivyo ujenzi wa maegesho hayo uende kwa kasi huku ukizingatia matakwa ya kiufundi na ubora wa hali ya juu.

Aidha Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Lindi ambao ni msimamizi wa mradi huo, Mhandisi Margwe Boay alionyesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo na kumtaka Mkandarasi kumaliza kazi hiyo mapema iwezekanavyo. Mhandisi Boay, alimhakikishia Dk. Mgwatu kuwa wataisimamia kazi hiyo kwa kadri ya uwezo wao ili Mkandarasi akabidhi kazi ndani ya muda uliopangwa.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Hematec Investment Limited inayojenga maegesho hayo Mhandisi Emmanuel Lyimo, amesema mradi huo utakamilika kwa wakati na kuahidi kuwa kufikia mwisho wa mwezi Juni ujenzi wa maegesho upande wa Lindi utakuwa umefikia hatua nzuri na hatimae kuendelea na ujenzi upande wa Kitunda

0 comments:

Post a Comment