Sunday 18 June 2017

Real Madrid watangaza dau la Ronaldo

Baada ya kuipa mafanikio makubwa klabu yake ya Real Madrid ya Hispania, Mshambuliaji wa Klabu hiyo Cristiano Ronaldo ameutaarifu uongozi wa klabu hiyo kuwa anataka kuondoka endapo atapata klabu ya kumnunua .

Cristiano Ronaldo

Hatua hii ya Ronaldo ambaye pia ni mshindi mara nne wa tuzo ya ‘Ballon d’or’ inakuja baada ya kupata kesi ya ukwepaji kodi wa kiasi cha Euro Milioni 13.

Klabu ya Real Madrid  kupitia Gazeti la Marca imetangaza kwa vilabu viwili vya Man United na PSG vyenye nia ya kunasa saini ya mkali huyo kuwa kama vitakuwa tayari kulipia Euro milioni 160 basi watamuachia Ronaldo aondoke.

0 comments:

Post a Comment