Thursday 15 June 2017

Mke wa Waziri Mkuu wa Lesotho auawa kwa kupigwa risasi


Maandishi ya Polisi yanayoonesha


Mke wa Waziri Mkuu wa Lesotho Lipolelo Thabane, amepigwa risasi na kuuawa.

Kuuawa kwa mke huyo wa Waziri Mkuu Tom Thabane kumeanza kuzua hali ya wasiwasi wa kisiasa nchini humo.

Msemaji wa Polisi Clifford Molefe amesema Bi.Thabane mwenye umri wa miaka 58 alipigwa risasi akiwa na rafiki yake Jumatano jioni wote wakirejea nyumbani nje kidogo ya jiji kuu Maseru.

Polisi wanasema haijafamika lengo la mauaji hayo, wakati huu uchunguzi ukiendelea.

Muaji haya yanakuja wakati Mkuu Waziri Mkuu Thabane akitarajiwa kuapishwa baada ya chama chake kushinda Uchaguzi wa Wabunge uliofanyika mapema mwezi huu.

Bi.Lipolelo amekuwa akiishi mbali na mume wake Thabane tangu mwaka 2012 baada ya wawili hao kutengana wakisubiri cheti maalum cha kutambua hatua hiyo.

Wasiwasi wa kisiasa umeendelea kushuhudiwa nchini Lesotho tangu mwaka 2014 baada ya jaribio la mapinduzi ya kijeshi.

0 comments:

Post a Comment