Thursday 15 June 2017

Korea Kaskazini ilimwachilia mwanafunzi mmarekani kwa misingi ya kibinadamu


 Otto Warmbier akitumikia kifungo cha miaka 15

Korea Kaskazini imethibitisha kuwa ilimuachilia mwanafunzi raia wa Marekani Otto Warmbier katika misingi ya kibinadamu.

Bwana Warmbier mweye umru wa miaka 22, alisafirishwa kuenda Marekani akiwa amepoteza fahamu siku ya Jumanne baada ya miezi 17 kizuizini.

Korea Kaskazini ilisema kuwa aliugua muda mfupi baada ya kuanza kifungo chake cha miaka 15 na kazi ngumu, kwa kujaribu kuiba bango la propaganda kutoka hoteli moja.

    Mwanafunzi aliyeachiliwa na Korea Kaskazini alazwa hospitalini

Alipewa tembe ya usingizi baada ya kuugua baada ya hukumu yake mwaka uliopita na hakuamka tangu siku hiyo, Korea Kaskazini ilisema.

Joseph Yun, mjumbe maalum wa wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Korea Kaskazini alisafiri hadi nchini humo na kikosi cha madaktari kuomba aachiliwe.

Madaktari walionekana wakimbeba mtu anayeaminika kuwa Warmbier

Familia ya Otto Warmbier ilisema kuwa hajapokea taarifa zozote kutoka kwake kwa zaidi ya mwaka mmoja na waliambiwa wiki iliyopita kuwa alikuwa amepoteza fahamu.

Bwana Warmbier pia anaamika kupigwa mara kadha akiwa kizuizini, kwa mujibu wa The New York Times.

    Mmarekani aliyekamatwa Korea Kaskazini atambuliwa

Korea Kaskazini ilitangazwa kuachiliwa kwake kwenye tearifa fupi iliyotangazwa na shirika la serikali la KCNA leo Alhamisi.

Lilisema kuwa bwana Warmbier amekuwa akifanya kazi ngumu na alirejeshwa nyumbani kwa misingi ya kibinadamu.

0 comments:

Post a Comment