Kutokana na jambo hilo, marefa watakaongoza michezo ya michuano hiyo wamepewa mamlaka ya kusimamisha na kuvunja mchezo ikiwa watathibitisha suala lolote la ubaguzi wa rangi katika FIFA Confederations Cup.
Uamuzi huu ni moja ya sehemu ya 3 ambazo zinampa mwamuzi nguvu ya kusimamisha mchezo mpaka kuuiharisha mchezo kabisa kutoka vitendo visivyo vya kimichezo vya mashabiki.
Chombo cha mamlaka ya juu ya soka kitaweka waangalizi wa vitendo vya kibaguzi.
“Hizi ni hatua tunazochukua kupambana na masuala ya ubaguzi kwenye soka,” – alisema Rais wa FIFA Gianni Infantino.
Mashindano ya mwaka 2017 ya Confederations Cup ni ya 10 tangu yalipoanza na hushirikisha bingwa wa kila bara, mshindi wa kombe la dunia na pamoja mwenyeji wa michuano.
0 comments:
Post a Comment