Mlipuko wawauawa watu 25 nchini Somalia
Idadi ya watu waliouawa katika shambulio lililotekelezwa na wapiganaji wa al-Shabab nchini Somalia katika migahawa miwili katika mji mkuu wa Mogadishu usiku uliopita imefika 25.
Wapiganaji hao waliwateka makumi ya raia kabla ya vikosi vya usalama kuwakomboa mapema siku ya Alhamisi na kufanikiwa kuwaua watekaji 5.
Ripoti sasa zimeibuka kwamba wapiganaji hao huenda walivamia hoteli tofauti na sio waliodhamiria.
Lengo lao lilikuwa mgahawa na kilabu cha burudani kwa jina Posh Treats uliopo barabara iliyopo mkabala ya jengo la Pizza House mmoja ya migahawa maarufu ya kisasa ambayo huuza chakula na burudani mjini Mogadishu na hutembelewa sana na vijana.
Wakaazi waliripoti kusikia milio ya risasi na milipuko katika eneo hilo usiku kucha.
Miongoni mwa waliouawa ni mpishi raia wa Syria ambaye alikuwa akifanya kazi katika mgahawa wa Pizza House.
Ni shambulio la kwanza kubwa tangu kuanza kwa mwezi wa Waislamu wa Ramadhan.
Katika wiki za hivi karibuni ,maafisa wa usalama wamekuwa wakitekeleza operesheni za kuwapokonya watu silaha katika mji mkuu wa Mogadishu.
Rais wa Somalia Mohammed Abdullahi Mohamed ameapa kuliangamiza kundi hilo katika kipindi cha miaka miwili.
0 comments:
Post a Comment