Thursday 15 June 2017

Hofu yatanda katika bandari Marekani kufuatia tishio la kuwepo kwa bomu


Walinzi wa pwani katika bandari ya Charleston upande wa South Carolina Marekani walilazimika kuondoa maafisa wa mamlaka ya bandari hiyo na wafanyakazi kufuatia ilani ya kuwepo kwa bomu katika mojawapo ya shehena .

Maafisa wa uslama wa pwani walifahamisha kwamba kuliwa na ilani ya kuwa na bomu katika meli ya Maersk Memphis iliyokuwa imeegeshwa katika bandari hiyo.

Tukio hilo limeripotiwa kutokea siku ya Jumatano majira ya jioni saa mbili na baada ya wafanyakazi kuondoka bandari hiyo walinzi walianza uchunguzi mara moja .

Meli hiyo inasemekana ilikuwa imetoka nchini Pakistan.

Baadaye idara ya ulinzi wa pwani kupitia twitter walifahamisha kwamba bandari hiyo ipo salama na kwamba hamna tishio lotote la bomu.

0 comments:

Post a Comment