Thursday 15 June 2017

DC SHINYANGA AFANYA ZIARA KATA YA DIDIA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO


Mbali na kutembelea miradi hiyo ambayo mradi wa maji wa visima virefu,zahanati ya Didia na Kituo cha Polisi Didia pia amezungumza na wananchi wa kijiji cha Chembeli kilichopo katika kata ya Didia. 

Matiro alikuwa ameambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Shinyanga lakini pia watalaam mbalimbali kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo,Bakari Kasinyo. 

Tazama picha za matukio yaliyojiri wakati wa ziara ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa ziara yake leo Alhamis June 15,2017 katika kata ya Didia halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini ambapo alisisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa ndani ya jengo la Kituo cha Polisi Didia ambacho kipo mbioni kukamilika ujenzi wake 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisilikiza maelezo kutoka kwa diwani wa kata ya Didia Luhende Masele ambaye alisema ujenzi wa kituo hicho unalenga kuwasogezea karibu wananchi huduma za kipolisi ili kukabiliana na vitendo vya kihalifu katika mji wa Didia ambao una wafanya biashara wengi 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama akiondoka na msafara wake katika kituo cha polisi Didia kuangalia jinsi ujenzi unavyoendelea .

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro leo Alhamis June 15,2017 amefanya ziara katika kata ya Didia halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini na kukagua miradi ya maendeleo. 

0 comments:

Post a Comment