Saturday 17 June 2017

China kujenga shule ya usafirishaji

Serikali ya China imesema kuwa ipo kwenye mazungumzo na Serikali ya Tanzania ya kujenga shule ya usafirishaji hapa nchini.

Akizungumza leo katika hafla ya kutoa ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu hapa nchini iliyoandaliwa na taasisi ya Confucius, Balozi wa China nchini, Dk Lu Youging amesema wakimaliza mazungumzo hayo wataanza ujenzi mara moja huku akisema lengo la ujenzi wa shule hiyo ni kuwaongezea ujuzi wahitimu na wale wasiokuwa wahitimu wa vyuo vikuu.

Aidha alisema kwa mujibu wa ripoti ya uwekezaji wa China hapa nchini ni kiasi cha dola bilioni saba huku kampuni zaidi ya 1,000 zikifanya shughuli zake na kutoa ajira 1,200 kwa Watanzania.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan aliyekuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo amezipongeza kampuni za China kwa kuisaidia Serikali kupambana na changamoto ya ukosefu wa ajira.

0 comments:

Post a Comment