Thursday, 23 March 2017

Viongozi wa Libya yawarejesha nyumbani wahajiri haramu kutoka Niger

Viongozi wa Libya wamewarejesha makwao makumi ya raia wa Niger ambao walikuwa njiani kuelekea barani Ulaya.
Badr al-Din Bin Hamad, mkuu wa ofisi ya kupambana na wahajiri haramu nchini Libya amesema kuwa, serikali ya nchi hiyo kwa uratibu wa Shirika la Kimataifa la Uhajiri, imeweza kuwarejesha makwao raia 159 wa Niger, watatu kati yao wakiwa ni watoto wachanga.
Wahajiri haramu wanaoelekea barani Ulaya
Kwa mujibu wa Bin Hamad, raia hao wa Niger wamerejeshwa nchini kwao kwa kutumia usafiri wa ndege.
Libya inahesabiwa kuwa eneo linalotumiwa na maelfu ya wahajiri kuelekea barani Ulaya wanakodhani kwamba wanaweza kupata maisha mazuri na ajira. Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, Libya imekumbwa na tatizo la wahajiri haramu na baadhi yao wamekuwa wakinaswa au kuokolewa katika pwani ya nchi hiyo.
Wahajiri

0 comments:

Post a Comment